ZILIZO KIKI (BONGO) 🚨
Club ya Simba Pamoja na Lake Energies leo hii wamezingua kituo cha kuuzia mafuta ya vyombo vya moto maeneo ya Mabibo Mjini Dae es salam, akizungumza kwenye hafla hio mkuu wa habari wa club hio amesema, “Hii ni bidhaa mpya ambayo Simba na Lake Energy tumeingiza sokoni. Bidhaa hii inaweza kutumiwa na Wanasimba na watu wengine. Lakini pia ni mpango maalumu wa kujitengenezea mapato. Kwa kufahamu kwamba uhitaji wa mafuta ni mkubwa nchini, Simba Sports Club tukaiona fursa kushirikiana na Lake Energy ili kuwahudumia Wanasimba lakini pia kuwawezesha kuchangia klabu yao lakini pia kwa Lake Energy kurudisha kwa Jamii.”
“Kwenye vituo vyote vya Lake Energies kutakuwa na namba maalumu au sehemu ya ku’scan’ na ukishaweka mafuta utawambia unalipa kwa njia ya mtandao iwe kwa benki au mitandao ya simu. Huduma hii inafanya kazi kwa njia ya mtandao tu na kila lita unayoweka kuna asilimia inakuja Simba.”
“Jukumu la kuipatia mapato Simba ni jukumu la kila Mwanasimba hivyo kuanzia sasa kwa kila Mwanasimba, kituo chake cha kuweka mafuta ni Lake Energies. Na ukilipa tumia njia ya mtandao, ukilipa kwa cash hiyo siyo yetu lakini ukilipa kwa mtandao tunapata chetu, tunakwenda kuwalipa kina Chasambi, kina Mpanzu wanakwenda kutufanyia ubaya.”- Semaji Ahmed Ally.
