STELLENBOSCH FC YAPATA PIGO KABLA YA MECHI DHIDI YA SIMBA SC

ZILIZO KIKI (AFRICA) 🚨

Baada ya uwezekano wa kumkosa mchezaji muhimu Devin Phili kwa mechi zao zilizobaki, Kocha Steve Barker amethibitisha kuwa wamewasilisha ombi kwa SAFA kumruhusu Phili kuchelewa kujiunga na timu ya taifa siku moja baadaye, ili aweze kushiriki kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Simba SC.

Hali hiyo imezidi kuwa ngumu kwa Stellies baada ya majeruhi wawili, Ashley Cupido na Bradley Mojela kutokuwepo. 

Mojela amepata jeraha baya la msuli wa paja na anatarajiwa kuwa nje kwa angalau wiki sita.

Katika juhudi za kuziba mapengo hayo, Barker anatumai Phili atasafiri nao kwenda Tanzania na kujiunga na kambi ya timu ya taifa baada ya mchezo huo

Aidha, Sage ambaye hakushiriki mechi ya hivi karibuni kutokana na kutopona kikamilifu, sasa ameanza kuonyesha hali nzuri na anatarajiwa kuwa tayari kwa mechi ya mwishoni mwa wiki.

“Kumpoteza Phili, pamoja na majeruhi wa Cupido na Mojela, si jambo zuri, lakini tunalazimika kupata suluhisho,” alisema Barker.