MAONI YA MDAU KUHUSU SAKATA LA DABI YA KARIAKOO

ZILIZO KIKI (BONGO) 🚨

Yanga baada ya kutolewa klabu bingwa ni kama viongozi wao walipata mshituko, walianza kuwaza ni kitu gani wata waambia wanachama na mashabiki.

Kwa vile hawa viongozi Wana wajua vizuri mashabiki na wanachama wa klabu hii wakaamua kuja na matukio ya ajabu ajabu Ili kuwaondoa mashabiki wao kwenye kuhoji ni kwanini timu yenye Pacome, Aziz Ki, chama, dube, Nzengeli n,k ishindwe kwenda robo fainali?

Viongozi walivyo wajanja wajanja wakaona waje na tukio la ndoa ya Aziz Ki na Hamissa, wewe hujiulizi ndoa inafungwa bila ya uwepo wa ndugu wa upande wa mume?! Hilo tukio liliwatoa kabisa wananchi kwenye kufikiria kuhusu kutolewa klabu bingwa.

Tukio la chasambi kujifunga goli, walilibebea bango mpaka mtu mwenye akili timamu ilikuwa ni lazima ufikirie ni kwanini yanga wanafanya vile, ila jibu ni kuwa lengo ni kuwasahaulisha wanacnchi kuhusu klabu Yao na kilicho tokea klabu bingwa.

Hata hili la kutaka point 3 ni mfululizo wa kujificha Ili wanachama wabaki Wana tazama zaidi matukio kuliko timu ilicho fanya kwenye mashindano ya CAF, Kwa Sasa viongozi wa Yanga Kila katukio kanako tokea Wana kabeba hasa na lengo kuu ni lile lile kuwasahaulisha mashabiki wao.

Viongozi wenyewe wa Yanga wanajua kabisa hakuna kitakacho tokea huko CAS zaidi ya mchezo kurudiwa.

Si mara ya kwanza dabi ya kariakoo kuahirishwa, Sasa inakuaje msimu huu Hawa viongozi waje na hizi siasa?

Sisemeagi timu nyingine ila kwa kuwa Hili linatuhusu na sisi Simba sc nimeona niwajuze wanasimba wenzangu mjue kwanini haya.

NB: NINI MAONI YAKO.