ZILIZO KIKI (AFRICA) 🚨🇹🇿
Vigogo wa Tanzania Simba SC, wataanza mipango ya kurusha yote yanayo fanyika nyuma ya pazia kupitia kwenye chaneli yao ya YouTube hatua kwa hatua.
Hii itafafanua kila kitu walicho kua wana kipitia wakati wa kampeni zao za Kombe la Shirikisho la CAF msimu huu na jinsi walivyofanikiwa mpaka kutinga fainali. Kuanzia hatua ya awali hadi walipo kwa sasa.
Pia wamepanga kufanya mahojiano na Raisi wa heshima wa klabu Ndg, Mo Dewji, Mkurugenzi Mtendaji, Wajumbe wa Bodi, viongozi wa TFF, Viongozi kutoka Wizara ya Michezo, wachezaji manguli na magwiji waliowahi ichezea klabu huko miaka ya nyuma, mashabiki wanaotambulika na baadhi ya waandishi wa habari wenye ushawishi ili kuzungumzia jambo hili la ajabu katikea kwenye historia ya Klabu.
Ni klabu ya Al Ahly pekee walio wahi fanya hivi barani Afrika walipotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hii inatarajiwa kupata maoni zaidi ya milioni 3 katika siku chache tu.
Klabu kubwa = mambo makubwa! 👏
#NguvuMoja 🦁