SINGIDA BLACK STARS KUFUATA NYAYO ZA AZAM

 ZILIZO KIKI (BONGO) 🚨

Ni rasmi Timu ya Singida Black Stars inatarajia kuzindua uwanja wake mkoani Singida, uzinduzi utafanyika Marchi 24 mwaka huu, kwa mchezo wa Kirafiki dhidi ya club ya Yanga SC. Uwanja huo unaitwa AIRTEL STADIUM ambao wao ndio wameujenga kwa kushirikiana na na makampuni mengine ya Azam, GSM, NBC, SBS na MO FOUNDATION. Nadhani ni wakati sasa kuwekwa hata sheria ya dharula kwa vilabu kongwe na vikubwa vya Simba na Yanga navyo vimiliki VENU zao, kwa maslahi mapana ya soka letu mana wao ndio mfano kwa wengine kwenye maswala mazima ya soka Nchini. Kongole sana viongozi wa SINGIDA BLACK STARS ✋