ZILIZO KIKI (AFRICA) 🚨
Mshambuliaji wa zamani wa Simba Sc, Yanga Sc, na nahodha wa timu ya taifa ya Uganda, 'The Cranes', Emmanuel Arnold Okwi ametangaza kustaafu soka la Kimataifa akiwa na umri wa miaka 32 akihitimisha uhudumu wake wa miaka 16 ndani ya Uganda 'The Cranes'. Okwi ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Kiyovu SC ya Rwanda alianza kuitumikia The Cranes mnamo 2009 akiifungia magoli 28 kwenye mechi 95 ambapo alipewa unahodha wa The Cranes mnamo mwaka 2021 baada ya kustaafu kwa aliyekuwa nahodha golikipa Denis Onyango. “Kuiwakilisha nchi yangu kwenye jukwaa la kimataifa imekuwa ndoto yangu ambayo imetimia kila mara iliacha hisia maalum, na kuwa nahodha wa timu yetu ilikuwa fursa na heshima kubwa.” ameandika Okwi katika taarifa yake ya kuaga.
