ZILIZO KIKI (AFRICA) 🚨
Baada ya siku ya jana kufanya mazoezi peke yake, hii leo Golikipa wa club ya Simba SC na Guinea Moussa Camara amefanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa ya Guinea, tayari kujiandaa na michezo ilio mbele yake. Camara yupo tayari kuwakabili Somalia, ambao watakutana Machi 21 katika mechi ya kufuzu World Cup 2026. Hizi ni habari njema kwa Guinea na Simba SC, all the best nyanda ya boli.
