MASHUJAA NA SALUM MAYANGA MAMBO SAFI

ZILIZO KIKI (BONGO) 🚨

Kocha Salum Mayanga anajiunga na Mashujaa FC akitokea Mbeya City ya NBC Championship. Kocha Mayanga msimu huu akiwa na Mbeya City ameingia robo fainali ya Kombe la shirikisho la CRDB kwa kumtoa Azam FC na pia yupo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Championship akiwa na alama 49 nyuma ya Mtibwa Sugar mwenye alama 54. Mashujaa imekamilisha taratibu zote za kumuajiri Salum Mayanga kuwa kocha Mkuu akichukua nafasi ya Mohamed Bares alie futwa kazi klabuni hapo, Mashujaa waliwasili Kigoma jana wakitokea DSM walipokuwa wakifanya mazoezi, pia kocha Mayanga atawasili Kazini leo Jumatano Machi 19 akitokea Mbeya City.