ZILIZO KIKI (ULAYA) 🚨
Kutoka London kwa Majogoo wa Jiji, msimu huu walikua wamoto sana na kila mtu alihofu kukutana nao, mwanzoni majogoo waliongoza kwa kila kitu ila taratibu walianza kunyong'onyea, ilianza FA walitolewa mapema tena na timu ya ligi ya chini, kukawa bado kuna matumaini kwani walibakiwa na nafasi 3 za kutwaa ubingwa msimu huu kwani walimaliza wakiwa juu kwenye msimamo wa champions league na vilevile walikua bado wapo final kwenye ligi ya Carabao, wakikwa bado na matumaini ya kutwaa ndoo ya Eufa, wakajikuta wanaondoshwa na wababe wa Ufaransa PSG kwa mikwaju ya Penalt, matumaini yakazidi kufifia, ila bado wanaume wakasema bado tuna nafasi mbili za kunyanyua kwapa hivyo tuendelee na mapambano, kwenye mechi ya final ya Carabao ilio wakutanisha na matajiri wapwa wa black and white (Newcastle United) majogoo wakajikuta wameangua tena pua, looh ! hii ni sawa na kisicho ridhiki na hatimae kabakiwa na nafasi moja tu pekee ya kutwaa EPL. Huku akiwa yeye ndio kinara wa ligi matumaini ni makubwa ila sijui kama bahati itakua kwao mana msimu huu kama bundi analilia langoni kwao. Poleni sana majogoo ila naamini EPL mtaishinda, hii ndio Football wakati unahisi kila kitu kipo upande wako, ghafla tu kimoja kimoja kinakutoka, hisis hii ukitaka kuijua vizuri kamuulize Kipara bwana PEP Gadiola atakua na majibu yote.
