JORGE JESUS ATAJWA KUCHUKUA NAFASI YA DORIVAL BRAZIL

ZILIZO KIKI (ULAYA) 🚨

Baada ya kumfuta kazi kocho Dorival Junior, timu ya taifa ya Brazil yatajwa kukaribia kutangaza kocha mwengine na jina lake ni Jorge Jesus, ana miaka 70 ni kocha kutoka nchini Ureno, anatajwa kuwa moja ya makocha bora kwenye ardhi ya Ureno. Amefundisha klabu mbalimbali zikiwemo Braga, Flamengo, Benfica, Fenerbahce na kwasasa anafanya balaa zito Al Hilal ya Saudi Arabia. Kocha huyo ameandikwa kwenye vitabu vya historia huko Brazil baada ya kushinda Copa Libertadores akiwa na Flamengo walipoifunga River Plates ya Argentina. Taarifa zinazovuma kwasasa ni kuwa kocha huyo mwenye maamuzi makali amekubali kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Brazil inayopitia nyakati ngumu kwasasa. Ifahamike kuwa Jesus amewahi kumfundisha mchezaji maarufu zaidi kwenye kikosi cha Brazil kwasasa Neymar wakati akikipiga Al Hilal na yeye ndiye alifanya maamuzi ya Neymar kuvunjiwa mkataba klabuni hapo. Bado Shirikisho la soka nchini Brazil halijafanya maamuzi kwani kocha wa zamani wa timu hiyo Tite nae anatajwa hivyo wataamua ni nani anakwenda kuchukua mikoba ya kikosi hicho muda wowote kutoka sasa.